sualogo

Mtandao wa Ushauri kwa Wakulima

(MUWA)Yaliyojili katika kilimo

kilimo shadidi cha mpunga

Kilimo Shadidi cha Mpunga au kwa Kiingereza ‘System of Rice Intensfication’ (SRI) ni mbinu ya kilimo ikolojia ya kuzalisha mpunga kwa njia ya umwagiliaji kwa kutumia maji kidogo na kupanda miche ya mpunga ikiwa na umri mdogo (siku 8-12 baada ya kuchipua). Kwa kutumia mbinu hii miche ya mpunga inapandikizwa kwa kutumia nafasi kubwa kati ya mche na mche. Umwagiliaji maji hufanyika pale tu udongo unakauka maji na kupasuka pasuka. Ili mbinu hii ifanikiwe, ni lazima uwe na uhakika wa kupata maji ya kumwagilia pale yanapohitajika. Kama maji hayatapatikana, matokeo yake hayatakuwa mazuri.

Utaalishaji wa udongo

Utunzaji wa udongo unategemeana kwa kiasi kikubwa na mazingira ya kibiolojia. Kazi kubwa ya baadhi ya viumbe hai waliomo kwenye udongo, ni kumeng’enya mabaki ya mimea na viumbe hai wengine. Mtiririko huu hufanya uwepo wa nguvu, virutubisho, na hewa ya kaboni, ambavyo kwa pamoja hutengeneza rutuba kwenye udongo. Utunzaji wa rutuba ya udongo unaongozwa na filosofia hii ‘Lisha udongo ili nao ulishe mimea.’ Udongo wenye rutuba utazalisha mimea yenye afya inayoweza kukabiliana na magonjwa. Uzalishaji wa mazao kwa njia za asili uhakikisha kunakuwepo uzalishaji wa kutosha bila ya kutumia pembejeo za ziada isipokuwa matandazo, mboji na bila kutifua udongo mara kwa mara. Ongezeko la malighafi za asili husaidia kuimarisha udongo na kufanya kuwepo kwa virutubisho vya kutosha.

Kilimo cha mtama

Mtama hutoa mazao mengi hata kwenye hali ambayo haifai kwa kilimo cha aina nyingine za mazao ya nafaka. Mtama una uwezo mkubwa wa kustahimili ukame. Mtama unastawis vizuri kwenye mazingira yenye wastani wa milimita 400 – 700 za mvua kwa mwaka. Pia mtama unavumilia sehemu zinazotuhamisha maji, na unaweza kulimwa sehemu zenye mvua nyingi. Mtaama unafaa pia kwa sehemu kame zenye wastani wa joto la chini kiasi cha nyuzi joto 18°C, ili kuweza kuota vizuri, na kiasi cha nyuzi joto 25-30°C ili kukua vizuri. Mtama hauwezi kuvumilia barafu. Mtama unaweza kukua kwenye aina zote za udongo. Kwa kiasi kikubwa unafaa zaidi kwenye udongo wa mfinyanzi, lakini pia kwenye udongo ambao una kiasi kidogo cha mchanganyiko wa kichanga. Mtama unaweza kuvumilia uchachu kwenye udongo kuanzia pH 5.0-8.5, na inavumilia udongo wenye chumvi kuliko yalivyo mahindi.

Ufugaji wa nyuki

Hatua zinazostahili kufuatwa unapoanzisha mradi wa ufugaji wa nyuki:- 1.Pata ufahamu wa uhusiano baina ya nyuki na mwanadamu katika eneo lako. 2.Jifunze namna ya kufuga nyuki. 3.Pitia visa kadhaa vya kung’atwa kabla ya kujitolea kufuga nyuki. 4.Unda utaratibu mzuri na ulioboreshwa wa ufugaji wa nyuki.